Breaking News
Loading...

Monday, 16 January 2017

Kikosi bora cha michuano ya Mapinduzi

Msuva - Bora
Baada ya klabu ya Azam kufanikiwa kunyakuwa taji lao la tatu la michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Mnyama kwa goli moja kwa bila
tunakuletea kikosi bora cha michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kudumu kwa takribani wiki mbili, na kushuhuhudia Azam wakitwaa Taji hilo la Mapinduzi.
Ndiye mlinda mlango bora wa michuano, Manula amefanikiwa kucheza mechi 5 bila kuruhusu goli lolote katika mashindano hayo, kipa huyo amekuwa bora kwa kuondoa michomo hatari langoni mwake hasa kwenye mechi ya fainali dhidi ya Simba
Mlinzi wa pembeni wa Msimbazi, Mkongo huyo ame imarika katika mashindano hayo ana kumbukwa kwa kufunga penati ya mwisho iliyo ipeleka klabu yake fainali dhidi ya Yanga 
Ameendeleza makali yake kama ya Ligi Kuu Bara, ndiye chachu ya mnyama kufika fainali kwani mchango wake ulikuwa mkubwa, mlinzi huyu amekuwa akizalisha magoli mengi kwa krosi zake maridadi
Ameibuka mchezaji bora wa mashindano, Mzimbabwe huyo alikuwa nguzo kwa klabu yake ya Simba, uzoefu wake umeifanya Simba kutotetereka kwenye eneo la ulinzi, katika mechi 6 za mashindano wameruhusu magoli mawili pekee
Ndiye mchezaji bora wa mechi ya fainali dhidi Simba, Morris amefanikiwa kutengeneza ngome nzito na kufanikiwa kutofungwa hata goli moja kwenye mechi 5 walizo cheza kwenye kombe hilo
Kiungo mkabaji wa klabu ya waoka mikate wa Azam, kingwa ni jina geni hapa nchini katika medani ya soka, amefanya kazi kubwa ya kuilinda ngome yake kutopitika kirahisi, mchezaji huyu ndiye aliyekuwa ana maliza kazi zote kabla ya kuwafikia kina Morris na wenzake
Mfungaji bora wa mashindano haya, ameibuka kinara wa mabao baada ya kufunga manne katika mechi 4, pia winga huyo amekuwa msaada wa kuzalisha magoli mengine kwa washambuliaji wake
Amefanya vizuri sana, kwa kuifanya Simba kuwa moja ya timu ngumu katika mashindano hayo, Mkude amecheza mechi zote za mashindano hayo ametengeneza uwiano mzuri kwenye klabu yake kwa kuifanya kuwa timu ngumu kufungika
9.Labama Bokota-U.R.A
Mfungaji bora namba mbili baada ya kutikisa nyavu mara 3 goli moja nyuma ya kinara Simon Msuva, straika huyu wa klabu ya URA ya Uganda amethibitisha ubora wake wa kufumania nyavu na nguvu za kuwasumbua mabeki
10.Said Mohamed-Taifa Jang'ombe
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Taifa Jang'ombe, Said Mohamed maarufu kama Messi wa unguja ameibuka mchezaji chipukizi wa mashindano hayo baada ya kuiwezesha klabu yake kutinga nusu fainali
Nyota huyu wa zamani wa klabu ya Mbeya City, amefanikiwa kufunga goli moja na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji wake kwa kupiga krosi nzuri

No comments:

Post a Comment