Breaking News
Loading...

Wednesday, 18 January 2017

Mbowe alaani kitendo cha polisi kumkamata Mh. Lowassa

Image result for mbowe 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe amelaani kitendo cha polisi mkoa wa Geita kumkamata mjumbe wa kamati kuu ya Chama hicho na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa.
Polisi hao walimkamata kipindi anaelekea katika kata ya Nkome jimbo la geita vijijini alipokuwa akienda kushiriki katika kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani.
Mh. Mbowe ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha kamati kuu ya chama hicho jijini Mwanza ikiwa ni siku moja tangu kukamatwa kwa Mh. Edward Lowassa.

No comments:

Post a Comment