Breaking News
Loading...

Thursday, 12 January 2017

Natamani Diamond na Kiba wasipatane

Image result for diamond and alikiba

kama wewe ni mshabiki wa kizazi kipya, ni lazima utakuwa na ufahamu kuhusu miambi miwili inayotamba hapa nchini hivi sasa; Diamond na Ali Kiba.


Kwa sasa hawa ndio mabalozi wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, bila wao pengine leo tungekuwa tunaqzungumza mengine kuhusu muziki huo

Miamba hawa wametengeneza aina ya ushindani katika mziki wa bongo na kufanya ushindani huo kuonekana kama uadui, ambao ni ushindani wa nani zaidi baina yao, ni ushindani ambao unaitajika katika muziki.

Kwa Tanzania mara ya mwisho kuwa na ushindani wa namna hii ilikuwa yapata miaka iliyopita. Kulikuwa na waigizaji wawili maarufuwa filamu hapa Tanzania, mmoja akiitwa Vincent Kigosi (Ray) na mwingine akiitwa Steven Kanumba(mungu marehemu)

Wasanii hawa walikuwa na ushindani mkali katika wakati ambao naweza kusema ulikuwa wa dhahabu katika tasnia ya filamu hapa nchini. Kila bbada ya miezi mitatu kulikuwa na filamu mpya kutoka kwa mmoja wao.

Ushindani wao uliibua kada ya watu walioitwa wasanii, kukaibuka vibanda vingi vya kuhuza filamu za kitanzania. Wakati wote huo Ray na Kanumba walikuwa wakiishi kama maadui, huyu akisema hili huyu anasema lile.

Tofauti ya ushindani wa Ray na Kanumba na huu wa Kiba na Diamond ni mitandao ya kijamii pekee. Wakati ule ushindani wao ulichangizwa zaidi na magazeti ya udaku lakini sasa mitandao ya kijamii inakoleza na inafika mbali zaidi kuliko magazeti.

Kwa bahati mbaya kwa tasnia, kanumba akatangulia mbele za haki, leo hii tangu kifo cha marhemu kanumba tasnia ya filamu imetetereka. Ray anaendelea kutoa filamu kama kawaida lakini bila ushindani, kuna ladha inapotea. Ni kwa sababu mtu aliyekuwa anamsukuma kufanya vizuri zaidi hayupo hata kazi zake za siku hizi zinaonekana hazikui. Zina kiwango kilekile kilichokuwapo kipindi kile Kanumba akiwa hai.

Ushindani wa Kiba na Diamond unakuza thamani ya mziki wetu. Kabla hajatoa wimbo wowote ni lazima wa hawa akune kichwa kujua utapokewaje na mashabiki pamoja na mshindani wake. Matokeo yake ni kwamba ubora wa kazi zao unaongezeka.

Ubora huo mkuongezeka maaana yake ni kuwa wanasababisha hata wasanii walioko chini yao nao waongeze ubora wa kazi zao, hivyo kinachoonekana ni ugomvi wa watu wawili walio juu kinasababisha maendeleo makubwa katika mnyororo mzima wa thamani katika tasnia ya muziki hapa nchini.

Nahitimisha kwa kusema kwamba kwamba upinzani huu mkali kati ya Diamond na Ali Kiba uendelee kama ulivyo au pengine uendelee kwa maana kwamba kama utaongezeka wote watapata mafanikio na waliochini yao watafanikiwa kwa kutaka kazi nzuri ili wafikie mafanikio waliofikia Diamond na Ali Kiba.

No comments:

Post a Comment