Katika sakata la kupambana na madawa ya kulevya jijini Dar es salaam, baada ya kuwashikilia baadhi ya watu wanaosadikika kujiusisha na madawa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametoa wito kwa wazazi wenyeviti wa mitaa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola juu ya watumiaji na watu wote wanaojihusisha na madawa hayo.
Akizungumza na Vyombio vya habari Mh. Makonda amesema, " naomba kusema haya, natoa siku kumi kwa kila mwenyekiti wa mtaa kwenye mitaa yote ya Dar es Salaam kutoa taarifa za mtaa wake juu ya dawa za kulevya. Natoa siku kumi kwa kila mzazi mwenye mtoto anayejiusisha na matumizi ya dawa za kulevya watoe taarifa kwa kamishina wa polisi, pia mkuu wa mkoa huyo ametoa siku kumi kwa mtu yeyote ambaye amewai kujiusisha na biashara au utumiaji wa dawa za kulevya kujipeleka wenyewe polisi kabla hawajatafutwa" alisema
No comments:
Post a Comment