Breaking News
Loading...

Monday, 6 February 2017

Msikilize mwenza wako anaposema ‘Nimechoka sana leo’ kwenye mapenzi



MARA zote maneno ya kuashiria uchovu katika uwanja wa sita kwa sita kama “sitaki sasa, mpenzi, nimechoka,” limekuwa likizungumziwa kwa muda mrefu na wapenzi ambao wanaonekana kuchoshwa na kile wanachoona kama kisingizio kwa upande wa wapenzi wao mradi tu wasifanye mapenzi. 


Utafiti uliofanywa kwa wanawake zaidi ya 93,000 umegundua kwamba, usingizi mzuri huongeza sana hamu ya kufanya mapenzi na hivyo kuwafanya wafurahie tendo hilo. 

Wale waliochoka, hata hivyo, walisema kuwa hawana furaha katika maisha yao ya kimapenzi. 

Utafiti uliofanywa na taasisi ya North American Menopause Society NAMS) ilifanya uchambuzi wa takwimu zilizopatikana kwa wanawake wenye umri  kuanzia miaka 50 hadi 79. 

Watafiti wanasema kwamba matokeo yanaonyesha kuwa upo uhusiano wa moja kwa moja baina ya usingizi wa muda mfupi, dalili za kukosa usingizi au insomnia na kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi baada ya wanawake kupita umri wa kuzaa, yaani menopause. 

Miongoni mwa wanawake walioshiriki katika utafiti huo, asilimia 56 walisema kuwa “wanaridhika kiasi” au “wanaridhika sana” na ufanyaji wa mapenzi, wakati kwa ujumla asilimia 52 walisema wamefanya mapenzi na wenza wao angalau mara moja katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. 

Chini ya theluthi moja ya washiriki walisema wanakabiliwa na matatizo ya kupata usingizi, ambalo ni tatizo kubwa kwa wanawake waliovuka umri wa kuzaa, yaani walioingia kwenye menopause, tatizo ambalo linaweza kusababisha shinikizo la damu na msongo wa mawazo. 

Utafiti huo pia uligundua kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya usingizi mzuri na wa kutosha na kuridhika kimapenzi hata baada ya kuhusisha mambo mengine ambayo yanasababisha ukosefu wa usingizi, kama msongo wa mawazo na magonjwa sugu. 

Wakati ukosefu wa usingizi hupunguza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake, hata hivyo haikupunguza idadi ya siku ambazo walifanya mapenzi na wenza wao, utafiti huo uligundua. 

Watafiti walisema kwamba tatizo sugu la ukosefu wa usingizi unamaanisha kwamba wanawake wanaweza kuendelea na shughuli zao za kila siku, ikiwemo kufanya mapenzi, lakini hali yao ya kufurahia na kuridhika nalo inapungua kutokana na kukosa usingizi. 

Dkt. Joann Pinkerton, Mkurugenzi Mtendaji wa NAMS, alisema, “Kuna njia kadhaa za matibabu kusaidia ukosefu wa usingizi na kutoridhika kimapenzi, ikiwemo pamoja na matumizi ya homoni, njia ambayo utafiti huo umegundua kwamba inafaa sana kwa wanawake ambao wameshapita umri wa kuzaa.” 

“Wanawake pamoja na watoa huduma za afya wanapaswa kutambua uhusiano baina ya dalili za menopause na ukosefu wa usingizi wa kutosha na jinsi zinaweza kuathiri furaha katika tendo la ndoa.”

Uhusiano huu baina ya kiwango cha usingizi na kufurahia tendo la ndoa unatofautiana kulingana na umri. 

Wanawake wenye umri mkubwa, kwa mfano, walikutwa kuwa na uwezekano mdogo kushiriki tendo la ndoa iwapo watalala chini ya muda wa saa saba had inane kwa usiku mmoja ukilinganisha na wanawake wenye umri mdogo, wakati wanawake wenye umri zaidi ya miaka 70 ambao wamelala chini ya masaa matano walikuwa na uwezekano mdogo zaidi wa kufanya mapenzi kuliko wale waliolala kwa kati ya saa saba hadi nane. 

Inafahamika kwamba uwezekano wa kuwa na matatizo ya kupata usingizi huongezeka kutokana na umri. 

Utafiti wa hapo awali wa Chuo Kikuu cha North Carolina uligundua kwamba hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake inaweza kuongezwa kwa kutumia dawa inayojulikana kama flibanserin, ambayo hapo awali ilitengenezwa kwa ajili ya kutibu maradhi ya msongo wa mawazo, ama antidepressant

Matokeo hayo yaliwafanya wanassayansi kusema kwamba dawa hiyo inaweza kuwa kama “Viagra kwa ajili ya wanawake.”
Utafiti mwingine mwaka jana pia uligundua kwamba wanaume wenye umri zaidi ya miaka 65 wanapaswa kufikiria juu ya kutumia matibabu ya homoni ili kuongeza hamu ya kufanya mapenzi, baada ya majaribio yaliyochapishwa katika Jarida la New England Journal of Medicine kugundua kwamba wale ambao walifanyiwa matibabu ya aina hiyo walikuwa na hamu zaidi ya kufanya mapenzi na pia walikuwa na furaha zaidi kuliko wazee ambao walikuwa na kiasi kidogo cha homoni maalumu kwa ajili ya mapenzi yaani testosterone
 
Pamoja na imani kwamba mwanga mdogo huweza kuwafanya wanaume wengi wakataka kufanya mapenzi, inadhaniwa kwamba wanaume wengi huweza kufanya mapenzi vizuri zaidi wakati kukiwa na mwanga zaidi, kitu ambacho pia kinaweza kuongeza kiasi cha homoni ya testosterone mwilini mwao. 

Hivyo basi, endapo mpenzi wako atakwambia kuwa amechoka na hawezi kufanya tendo la ndoa, ni vyema kumwelewa na kutokasirika kwa kuwa akiweza kupata usingizi mzuri utaweza kupata mambo mazuri na matamu zaidi siku zijazo. 


Makala hii imetafsiriwa kutoka Gazeti la The Telegraph la nchini Uingereza

No comments:

Post a Comment